Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ghuba hii yenye rangi ya zumaridi tangu zaidi ya miaka 550 kabla ya kuzaliwa kwa Nabii Isa, ilikuwa ikijulikana kama Ghuba ya Uajemi, katika kipindi ambacho nasaba ya Kuroshi (Cyrus) ilikuwa ikitawala Iran ya wakati huo, ambayo ilienea kutoka India hadi pembezoni mwa Ulaya ya Magharibi.
Daima, kila serikali iliyokuja kuongoza nchini Iran imekuwa ikitetea jina la “Ghuba ya Uajemi” kuwa ndilo jina halali pekee la ghuba hiyo. Jaribio la Trump la kupendekeza kubadilishwa jina hilo lilikuwa ni dai lisilowezekana, na likasababisha Wairani kutoka kambi zote za kisiasa kuungana pamoja na kulaani kauli hiyo kupitia matamko yao na machapisho katika mitandao ya kijamii. Katika nyakati za nyuma pia, Marekani imekuwa ikilitambua jina hilo la “Ghuba ya Uajemi” katika shughuli zake za kijiografia na kibiashara.
Turaj Darayee, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Kifarsi katika Chuo Kikuu cha California alisema: “Jina la ghuba hii liko juu ya mipaka ya kisiasa na itikadi za kidini; hakika jina hili linahusiana na taifa fulani na historia ya taifa hilo.”
Ahmad Zeydabadi, mmoja wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa, alichapisha katika mtandao wa X: “Kwa sababu tu ya matamanio na matakwa ya Trump, Ghuba ya Meksiko haiwezi kuwa Ghuba ya Marekani, Kanada haiwezi kuunganishwa na Marekani, Greenland haiwezi kutwaliwa na Marekani, na Ghuba ya Uajemi haiwezi kupewa jina bandia.”
Maoni yako